KUJENGA KWA MTINDO WAKE NA MBUNI YAKE

MAISHA YA PAMOJA YA KILA SIKU

Ndiposa iwe Nyumba nzuri ya Yesu kuishi, Nyumba ya Mungu lazima ijengwe pamoja kwa kutumia Mtindo Wake na Mbuni Yake. Nyumba Yake ina watu, Mawe yake yaliyohai, na ana njia ya pamoja ambayo lazima tujenge maisha yetu. Maandiko humwita Yesu Mjenzi Mkuu. Tunastahili kujali sana kuhusu Ramani Yake, Mpango Wake.

7/5/2006

Sasa kwa kuwa tumefafanua nyenzo nzuri za ujezi wa Nyumba ya Mungu ni nini …zingatia hii: Kisia tuchukue mawe yote mazuri, mbao zote nzuri, na nyenzo zote nzuri, zinazofaa za ujenzi ambazo Yesu amechagua kwa ajili ya Nyumba Yake na tuweke nyenzo hizo zote nzuri kwa fungu. Kisia nini? Bado hatuna nyumba. Nyumba ya Mungu inahitaji zaidi ya nyenzo nzuri za ujenzi (Wakristo wa kweli). Kwa sababu una nyenzo zote za nyumba zilizorundikwa katika fungu haimaanishi kwamba una nyumba ya kulala. Fungu hilo halitakulinda kutokana na dhoruba, haijalishi vile nyenzo hizo zinaweza kuwa nzuri.

Ndiposa iwe Nyumba nzuri ya Yesu kuishi, Nyumba ya Mungu lazima ijengwe pamoja kwa kutumia Mtindo Wake na Mbuni Yake. Nyumba Yake ina watu, Mawe yake yaliyohai, na ana njia ya pamoja ambayo lazima tujenge maisha yetu. Maandiko humwita Yesu Mjenzi Mkuu. Tunastahili kujali sana kuhusu Ramani Yake, Mpango Wake.

Mungu ana watu wengi wazuri ulimwenguni kote. Kile ambacho kimetendeka mara kwa mara katika miaka 2,000 iliyopita ni kwamba watu hawa wamekuwa wakitamani kubadilisha maisha yao na kumpendeza Yeye, lakini wametatizwa. Wameshindwa kupata uwezo wao wote na kwa kweli kumtumikia vizuri. Ni moyo wao wote, lakini wanashindwa tena na tena. Sababu ya hao kushindwa ni kwa sababu mara kwa mara tunajenga kwa njia isiyofaa. Hatujajenga kulingana na mtindo, mbuni, ambayo Mungu ametupa. Wakati mtu yeyote anapojaribu kitu chochote, lakini anajaribu kukifanya kwa njia isiyofaa kabisa, ni nadra yeye hufaulu, haijalishi vile yeye ni mwaminifu.

Nyumba ya Yesu imejengwa kwa mtindo Wake, sio wetu. Na mtindo Wake ni “baba, mama, ndungu, na dada mia moja.” Mtindo wake ni kuwa tuweze “kukiriana dhambi zetu” na tuponywe. Mtindo Wake ni kuwa tuweze “kuchukuliana mizingo na kwa hivyo kutimiza sheria ya Kristo.” Mtindo Wake ni kuwa tuweze kuwa “kitu kimoja, kama vile Yeye na Baba ni kitu kimoja.” Haja ya Mungu si mawe ya kando ambayo huja pamoja siku ya Jumapili ili “kuhudhuria” hotuba au karamu, lakini haja Yake ni familia ambayo imejengwa kwa pamoja kila siku, iliyounganishwa katika maeneo yote ya maisha ya kila siku, kama Familia.

Yesu amechagulia Nyumba Yake mtindo ambao unafanana katika kila nchi, haijalishi lugha au utamaduni. Mtindo huo ni kuwa watu wote wa Mungu watoe maisha yao kwa ajili ya kupendana na kuhudumiana kila siku, kama Familia, kwa pamoja. Kanisa la kweli la Yesu, liliunda njia Yake iwe yenye nguvu, lazima iwe Familia kila siku. Wanakula pamoja kutoka nyumba hii hadi nyumba ile nyingine, wanatumikiana na kusaidiana kwa njia nyingi kila siku. Wanazungumza neno la Mungu wao kwa wao kila siku ili kuwasaidia kuwa zaidi kama Yesu. Wanapoona dhambi, wanaenda kutembea na kuzungumza kuihusu kwa pamoja. Hawasubiri “Jumapili” ili wasikilize mtu akihubiri mahubiri kuihusu. Kusudi la Mungu (Waef. 3:10, 1Petro 2) ni kuwa sisi wote ni makuhani wa kila siku na wajumbe wa Mungu kwa yule mwingine “tunapoinuka, kukaa chini, na kutembea njiani.”

Sisi wote tumeitwa kuwa makuhani wa Yesu. Sisi wote tumeitwa ili kubeba neno la Mungu na kusaidiana. Hii inamaanisha kwamba ukimwona jirani yako akiwa mchoyo au mwenye hasira, au ukimwona akinywa, au mwenye kiburi ambacho kinavunja moyo wa Yesu, basi kila mmoja wetu atachukua jukumu la kusaidiana ili tubadilike. Hii ni ya kila siku. Haina lolote na kufanya na Jumapili. Kanisa la kweli la Yesu limeundwa na Mawe yaliyo hai, na mtindo wa Nyumba hiyo ni Familia ya kila siku. Si jambo ambalo “tunahudhuria,” bali ni vile tulivyo kila siku.

Je! unaona vile hizi zote zinaunganika? PAMOJA NA MAHUSIANO YA KILA SIKU TU ndio unaweza kujua ikiwa kuna mtu anayependa Nuru na Kweli, na kwa hivyo ni mtoto wa Mungu. Mikutano chache kwa wiki haitamruhusu mtu yeyote kujua ikiwa mtu anapenda Nuru na ana udhaifu, au ikiwa anachukia Nuru na kwa hivyo hajaokoka. Mpango wa Mungu ni hazina katika vyombo vya kidunia. Mpango ya Mungu ni ukuhani wa waumini. Mpango wa Mungu ni ya watu Wake ili “waonyane kila siku.” Kwa kweli tunapokuwa tukiishi hivi kwa pamoja, faida moja ni kuwa watoto wote wa kweli wa Mungu wanakomaa zaidi na zaidi. Matokeo mengine ya kutembea kwa pamoja kama vile Mungu alivyokusudia ni kwamba ikiwa mtu hapendi Nuru, hivyo basi anafichuliwa kama mnafiki. Ikiwa hawezi kurekebishwa, ikiwa hajali yale Yesu anasema kuhusu mambo haya, ikiwa anakasirika na ni mkatili, basi anafichuliwa kama Mkristo wa uongo. Inakuwa wazi kwamba lazima hakuwa kwa kweli ametoa maisha yake kwa Yesu kwa sababu ukweli ni kwamba mtu hawezi kuwa na Roho Mtakatifu na asipende Nuru (Yohana 3, 1Yohana 1, 3).

Tukijenga kwa njia hii—kwa kubadilisha maisha yetu ya uchoyo au ya uzembe, na kwa kweli kujifunza vile ya kupendana kama familia kila siku, kwa kuchukua jukumu la kutumikiana na kusaidiana na neno la Mungu—basi itakuwa Nyumba ambayo Yesu anaweza kuishi ndani na anaweza kuipenda. Itakuwa Nyumba yenye mbuni nzuri ambayo itakuwa rahisi kwa Yesu na kwa sisi wote kuishi na kufanya makao yetu.

Yesu alisema kwamba wakati tunapotumia neno Lake, wakati dhoruba inapokuja (na itakuja), basi nyumba hiyo itasimama. Itasimama kwa sababu imejengwa juu ya mwamba “kwa kutumia neno Lake,” sio kwa kufikiria au kuimba kuhusu neno Lake. Tukiimba juu yake tu, kuomba juu yake na kuzungumza juu yake na tusibadilishe vile tunavyoishi ili tutii neno Lake pamoja na yule mwingine, basi wakati dhoruba inapokuja, haijalishi vile nyumba hiyo inavyoonekana maridadi, itaangushwa na kuangamia. Hii ndio Yesu aliahidi katika Mathayo 7. Kwa hivyo, hakikisha umejenga njia Yake na unafanya jambo kuhusu Kweli Yake. Zitii, na kisha dhoruba haitakuumiza.

Kwa njia ile ile ndege ndogo au sungura mdogo hujificha chini ya mwamba wakati dhoruba inapokuja, unaweza kujificha katika makao ya bawa la Yesu ikiwa utajenga vile anavyokuagiza. Dhoruba itatikisa miti na kusongeza vitu vizito. Itaziangusha na radi itapiga. Lakini kama utajenga kwa njia ya Yesu na umtazame Yeye wakati inapokuja, utakuwa salama katika makao ya mabaya Yake. Dhoruba nzito itapita na jua litang’aa. Ndege wataanza kuimba tena, na maisha yatakuwa safi na mapya. Itakuwa nyumba yenye nguvu sana na yenye Mbuni nzuri. Wakati dhoruba itakapokuja na kugonga Nyumba, itasimama kwa sababu ina nyenzo nzuri tu, na kwa sababu mbuni ni nzuri. Kutakuwa na uharibifu mdogo sana kwa Nyumba hii nzuri, na sisi wote tutakuwa salama. Kama vile Baba alikuwa dhahiri kuhusu nyezo na mbuni Nuhu alistahili kutumia ili kujenga Safina, hivyo pia Yesu ana mpango wa nyenzo na mbuni ya Nyumba Yake. Na Mpango Wake si, katika Makubaliano Mapya, mtu mtakatifu akitoa hotuba kwa shirika la watu “wanaohudhuria” ambao wametenganishwa. ni SASA “wamama, ndugu, dada mia moja”—kila siku wakiunganishwa katika uhusiano wa ndani wa wapenda Nuru “kuanzia mdogo hadi mkubwa”.

Hii ndiyo Habari Njema ya Ufalme wa Yesu. Alisema, “Baba Yangu anabidii ya nyumba inayojengwa.” Baba anataka sana tujenge Nyumba Yake kwa njia Yake. Katika nchi nyingi na miji ni nadra sana nyumba kujengwa vile Yesu anataka ijengwe. Karibu katika kila “kanisa” karibu katika kila nchi, kuna watu wanaokuja pamoja na mila na tamaduni na kisha kwenda kivyao wakiishi maisha yao vile watakavyo. Pengine wanatenda dhambi, au pengine wanajaribu wasifanye dhambi. Lakini sio nyumba kwa sababu hao sio Familia, kila siku, kwa pamoja.

Ni wakati tu mawe yote yanapowekwa pamoja, na gundi la upendo wa kweli na uwezekano wa kudhuriwa, na kujengwa na mbuni ya Mungu, ndio inaweza kuwa mahali ambapo anaweza kupaita nyumbani. Hata kama wewe ni jiwe zuri lililohai na unajaribu kuishi maisha matakatifu, bado wewe ni jiwe moja. Nikiweka jiwe hilo mchangani, bado halitakuwa nyumba ya Yesu. Hataki mawe mazuri ya kibinafsi yakae uwanjani. Tunastahili kufanya sisi wenyewe, hata kama nikujilazimisha, tukae pamoja na mawe mengine. Kila siku lazima tujiamrishe kwamba tukae pamoja na mawe yale mengine, kila siku kwa mbinu ya Mungu ya Nyumba…tunapokuwa “tukiinuka, tunapokaa chini, tunapotembea barabani” kwa pamoja. Kuosha nguo kwa pamoja, na kwenda sokoni pamoja. Tunapofanya kazi mashambani, kutengeneza matofali, kukata mbao za kuni, au kutengeneza chakula, tufanye hivyo kwa pamoja ili tuwe Familia moja badala ya watu wengi au familia nyingi. Ni katika maswala haya “yasiyo na maana” ya maisha ya kila siku ambayo tunashikanisha Imani, Tumaini, na Upendo pamoja. Kazi hizi za kila siku, tukiishi kwa pamoja kama Familia, ndio “madirisha ya nafsi” ambayo huturuhusu sisi kujiosha na maji ya Ulimwengu, badala ya dini ambayo hufanya-iaminike ya “kuhudhuria” karamu za kidini na kuimba—pamoja na hotuba za mtu mtakatifu. Yesu hajengi chochote bali familia.

Yesu alisema, kwa kweli ukitii mapenzi Yangu, utakuwa na baba, mama, ndugu, dada mia moja—sio jirani mia moja, bali washirika mia moja wa karibu sana wa familia. Hii ni mapenzi ya Mungu. Haya ni mafunzo ya Yesu Kristo—kwamba ajenge nyumba Yake na nyenzo nzuri. Nyenzo mbaya hazikaribishwi ikiwa hazitabadilika wakati zinaposikia maneno ya Yesu.

jesuslifetogether.com
Kiswahili Languages icon
 Share icon