KUJENGA NA NYENZO NZURI

JE! KANISA NA MKRISTO NI NINI?

Kanisa la kweli lililojengwa na mawe yaliyo hai ambalo Yesu anaangalia na kulipenda lazima lijengwe na nyenzo nzuri.

7/5/2006

Biblia inafunza kwamba Mungu haishi katika nyumba zilizojengwa na mikono ya mwanadamu. Waefeso 2 pili na vifungu vingine vingi vya Biblia vinasema kwamba sisi ni nyumba au makao ya Mungu kwa Roho—Kanisa. Unapotembea au kuendesha gari barabarani, unaweza kutambua jengo la kidini kwa sababu linaonekana kama jengo la kidini. Bali, kwa kuwa Kanisa la kweli ni watu, na wala sio jengo, basi kwa kweli linafanana aje? Unawezaje kutambua t0fauti kati ya Kanisa la kweli na la uongo?

Katika “kanisa” la Agano la Kale, unakuwa mshirika kwa sababu ya vile wazazi wako walivyokuwa (Wayahudi). Ikiwa kwa kawaida uliamini jambo adilifu na wazazi wako walikuwa sehemu ya kanisa hili, na wewe “ulihudhuria kanisa” mara kwa mara na kutoa fungu la kumi, hivyo basi ulikuwa mshirika wa “kanisa.” Katika Kanisa la Yesu la Agano Jipya, hii si kweli—lazima utoe roho yako kwa Mungu. Unabii kuhusu Agano Jipya ulisema kwamba kanisa ambalo Mungu hujenga (Yer. 31, Waeb. 8, Waeb. 10) ndilo Kanisa la kweli, na kuanzia mdogo hadi mkubwa, washirika wake WOTE watamjua Mungu Aliyehai. Kanisa linaweza kufahamika kwa njia hii TU. Chochote chini yake kinaweza kumaanisha vyema na kufanya mema na ya kidini (ikihusisha watu wengine ambao Wameokoka), lakini SI kanisa la Yesu Kristo, jengo la mtaani, ikiwa tu ni watu “wanaohudhuria” kitu kilichopangwa kwa kalenda bila kuunganisha kila siku Maisha ya pamoja (1 Wak. 12).

Kanisa la kweli lililojengwa na mawe yaliyo hai ambalo Yesu anaangalia na kulipenda lazima lijengwe na nyenzo nzuri. Ikiwa jengo lolote limejengwa na nyenzo mbaya, unajua kwamba litaanguka. Ikiwa mbao ambayo imeshikilia paa imeoza, itaanguka. Matofali ambayo ni mepesi, yaliyoundwa vibaya, au yaliyoundwa na nyenzo mbaya hayawezi kumudu uzito na yataanguka. Vivyo hivyo, tukijaribu kujenga nyumba ya Mungu na nyenzo mbaya, hiyo pia itaanguka. Ikiwa mtu kwa kweli hamjui Mungu, hawezi kuwa mshirika wa Kanisa la Yesu. Ikiwa nyumba ambayo Mungu anajenga kutoka kwa wanaume na wanawake itaweza kusimama, ni lazima isiwe na mawe mbaya ndani yake (1 Wako. 3-5).

Kwa hivyo, je! Ni lazima Kanisa, au watu wake wawe wakamilifu? Kwa kweli hiyo haiwezekani (1Yohana 1). Lakini kulingana na Neno la Mungu, kinachohitajika ni hiki: Asilimia mia ya washirika..“wanapenda Nuru” na “wanapenda Kweli” na kwa hakika wamemuona Mungu Mwenyewe kwa njia ambayo “mnofu1 na damu haijafunua.” NDIO, hii inahitajika (Mat. 16:16-18, Yohana 3:19-21, 1Yohana 1-3, Eze. 11:19, Eze. 36:26, Yer. 31:34). Hayo ndio Yesu alisema atajenga Kanisa LAKE juu yake, ikiwa litakuwa Kanisa LAKE. Kitu kingine chochote kitakuwa kama kujenga nyumba na tofali nyepesi au mbao iliyooza. Nyumba ambayo Yesu anatengeneza ndiyo nyumba nzuri kabisa ulimwenguni, na Yesu atatumia nyenzo za kweli na nzuri tu ili kujenga Nyumba Yake.

Mara nyingine, hii HAIMAANISHI kwamba kila mtu ni mkamilifu. Bali, inamaanisha kwamba kila mtu anataka kumpenda na kumtii Yesu na hapuuzi usaidizi kutoka kwa wengine ambao wanataka kumsaidia kumpenda na kumtii Yesu; wanataka usaidizi huo. Nyenzo nzuri za ujenzi wa Nyumba ya Mungu ni wakati mtu “anapenda nuru”, kulingana na Yesu Mwenyewe. Nyenzo mbaya za ujenzi, kama vile mbao iliyooza, ni mtu ambaye hataki usaidizi huo. Mtu huyo husema, “Usinihukumu. Shughulika na mambo yako.” Hao husema kwa kujitetea, “Toa gogo lilioko kwa macho yako mwenyewe.” Hiyo ni nyenzo mbaya ya ujenzi, ambayo Mungu alisema haikubaliki katika Nyumba Yake. Yesu hatajenga nyumba Yake kwa njia hiyo. Hiyo ni mbao iliyooza na itakatwa kabisa kutoka kwa watu (Matendo ya mitume 3:23, Mat. 18, 1Wak. 5). Katika kanisa la Kweli, mtu anayefanya hivyo hajakaribishwa. Haijalishi pesa wanazo au vile wanavyofahamu Biblia zao vyema. Wanaweza hata kuwa “viongozi,” lakini ikiwa hawataitika kwa wepesi kwa mafunzo ya Yesu, hivyo basi hawawezi kuwa sehemu ya Kanisa la kweli la Yesu ambalo linajengwa Kiroho. wakikataa upendo na maombi, hekima, usaidizi na uvumilivu, basi kuwaruhusu waendelee kuwa kati ya watu wa Mungu itakuwa kumpinga Yesu na pia kupuuza amri Zake.

Ikiwa mtu ameokoka, ATAKUWA na Roho Mtakatifu (War. 8:9, Wag.3, Waef. 1). Na DHIBITISHO kwamba ana Roho Mtakatifu ndani yake (haijalishi ni mara ngapi amekuambia “ushuhuda” mkubwa na kusema, “Bwana, Bwana!” Mathayo 7) ni kuwa anapenda kutii. Hao ni viumbe vipya na sasa wanapenda Nuru, na wanapenda Kweli (2Wathe. 2:10), na “kama watoto waliozaliwa ” “wanatamani” Neno la Mungu litumike katika maisha yao (1Petro 2). Ikiwa mtu ana Roho Mtakatifu, atapenda Nuru na atapenda Kweli…. na kisha tabia yake itaanza kubadilika. Atatubu kwa jinsi anavyomshughulikia mume wake au mke wake, na atabadilika. Atatubu kwa jinsi anavyowashughulikia wafanyakazi wenzake, au watoto wake, au majirani wake, na atabadilika. Atatubu dhambi zake za zamani na tabia zake mbovu, na atabadilika na atakuwa amekomaa zaidi.

Kipawa cha Roho Mtakatifu ni stakabadhi ambayo inadhibitisha urithi wake. “Huu ndio uamuzi,” asema Yesu, katika Yohana 3. Hii ndiyo inatofautisha kutokuwa na hatia na kuwa na hatia. Si kwamba kila mtu ni mkamilifu, lakini wale WOTE ambao dhambi zao zimesamehewa “wanapenda Nuru.” Wanakipawa cha Roho ambacho hawakuwa nacho zamani. Sasa, kutoka ndani, mioyo yao ya jiwe imefanyika mioyo laini ya nyama. Kutoka ndani, Mungu anawasababisha kuweka amri Zake na makataa. Kutoka ndani, wanajali kuhusu maneno ya Yesu kuhusu tabia zao. Kondoo hujua sauti ya Mchungaji kwa sababu wana Roho ya Yesu. Kondoo husema, “Ninataka kumfuata Yesu! Niongoze njia hiyo.” Mbuzi husema, “Achana na mimi! Ninaweza kufanya miujiza! Ninaweza kupeana pesa zangu kwa masikini! Ninajua mambo. Mimi ni mzuri kukuliko, na sijali unachosema.”

Mkristo, mshiriki wa Agano Jipya, anapenda Kweli (2 Wathes. 2:10) na anapenda Nuru (Yoh. 3:19-21), na sasa ni “mshiriki wa asili KUU ” (Petr. wa pili mlango wa 1:4, War. 6:1-14). Hilo ndilo dhibitisho kwamba Roho anaishi ndani yao au kati ya mmoja wetu yeyote. Si lazima tuchukue neno la kila mtu kwa sababu anasema, “Bwana! Bwana!” Ni mtu yule aliyewacha nafsi yake na maisha yake kwa ajili ya Yesu TU, na Ameguwa na Mbingu na Muumbaji wa Ulimwengu anaishi ndani yake ndiye kwa kweli ameokoka, na ni “mshirika” wa Kanisa Lake la mtaani (War. 8:9-11, Lk. 9:57-62, Yoh. 1:12-13, 3:16-21,1 Yoh. 3:8-10, 5:18-20).

Jengo la Kweli, Kanisa halisi, LIMEDHIBITIWA NA wale ambao wamekuwa na ufunuo wa Mwana “ambao nyama na damu haikufunua (yaani asilimia 100 ya “washirika”!), bali Baba Mwenyewe aliye Mbinguni aliwafunulia.” Si kuhusu kukaribiana au ufahamu au “kujitolea” au malezi. Ni kuhusu kukabiliana kibinafsi na Mungu Baba, katika Utu wa Mwanawe, ambapo mauti hutoa aina ya Uzima wa Mungu, Maisha ya Zoe, kutoka kwa kitu kisichopo (Yoh. 3:5-8, Yoh. 12:24, War. 6:1-14, Wag. 6:14-17). Kwa kweli kuna wachache wanaohitaji “ustarabu maalum” na wengine ambao wanaamua katika “mwaka wao mmoja zaidi” (Yohana 13:8-9, Yohana 15, 1Yohana 2:19, Yuda 11-25).

Aidha, tuna maisha YASIYO ya kawaida na Yeye na sisi kwa sisi, au SI Ukristo wa Kibiblia na SI Kanisa halali. Kwa hakika kuna watu wengine ambao Wameokoka “wanaohudhuria” mashirika ambayo kwa kweli si makanisa, ijapokuwa wanajiita makanisa. Hilo ni suala tofauti. Kwa urahisi tunasema kwamba hatutagusa Kiti Chake cha Enzi (tutaguza tu hisia zisizo dhahiri za “akili” yetu) ikiwa hatutaishi Pamoja kila siku—Maisha ya ZOE—muda baada ya muda tukiunganishwa kwa Kichwa na yule mwingine! Karamu ya “huduma” ambayo “inafanywa kwa heshima Yake,” au kujifunza kweli kumhusu yeye, au kuita hisia kutoka Mbinguni na muziki wetu—kihistoria, hizi zimebadilisha maisha machache sana kuwa Mfano wa Mwana. Aidha tunashiriki katika Nguvu za Kichwa cha Mungu kwa pamoja kila siku, au sio Maisha ya Milele, au Jengo na Kanisa, kama vile Mungu atakavyo. “Chachu ndogo huchachua mkate MZIMA.”

Lazima tusiwe watoto tu ambao husema mambo yanayofaa, na hatuishi kama Yesu. Na, Kanisa sio mkusanyiko wa Wakristo wa uongo ambao wanasema mambo yanayofaa lakini hawana Roho wa Yesu anayeishi ndani yao, kama Mtu. Yesu ni Mjenzi mkubwa. Hatajenga na mawe mepesi au mbao iliyooza. Anataka kujenga Nyumba ya kuishi yenye Utukufu—moja ambayo inamfaa Mfalme kama Alivyo. Kwa hivyo nyenzo za ujenzi katika Nyumba ya Mungu lazima ziwe nzuri kabisa. Kanisa la kweli lililojengwa na Mungu, wala sio mikono ya mwanadamu, limejengwa na mawe yaliyohai—Wakristo wa kweli—kinyume na mawe yaliyokufa, matofali au nyasi. Yesu atajenga tu na nyezo nzuri za ujenzi . Ikiwa ametuoa katika Agano na Kiapo, tukawaacha wapenzi wale wengine wote, tukazaliwa mara ya pili, tuna mioyo nyepesi, tunapenda mafunzo Yake, kwa kweli tunataka kubadilisha mambo katika maisha yetu ambayo yanahitaji kubadilika, na tuelekeze nyuso zetu Kwake wakati wa shida au ugumu, tukimuuliza Yeye na ndugu na dada zetu kutusaidia sisi, basi sisi ni mawe maridadi yaliyohai ya Nyumba ambayo Yesu anaishi. Tunaweza na tutakuwa Bi-arusi wa Yesu wenye utukufu. Hii ndiyo Habari Njema ya Ufalme wa Mungu.

jesuslifetogether.com
Kiswahili Languages icon
 Share icon