Mwaliko Wake
Alikuja kutupa maisha kikamilifu—Kuishi maisha yake kilasiku kati yetu, sio kutamka maneno yaliyo ombwa, kuimba nyimbo na kuomba maombi yalivyo ombwa, kuimba nyimbo na kuomba maombi yalivyochafuliwa k.m. kioo kilichochafuliwa.MAISHA!
7/5/2006
Kutoka wakati wa mwanzo, ualiko huu umeleta watu kumtafuta Yeye.Ualiko huo Wake ni kwetu pia.Na hayo ndivyo yalivyo. Hii si funzo la nje.Ni mchoro na kuhadaa yale yaliyo ndani yetu. Ni sisi kutazama kwa yale yote ambayo ni Yeye Anayoyasema.
Siwezi kuishi bila Yeye au na yale yaliyo mazuri na muhumu Kwake. Sitaki kuishi bila hayo! Singependa kuota kuishi nje ya Mapenzi yake kwa maisha yangu au nje ya sababu Zake. Nataka kumfuata Mwana kondoo popote aendapo. Chochote Anachotaka kwa maisha yangu, Anacho! Ni mkate wa uzima,ambapo uhakika wangu wote na umefanywa kupatikana. Ni picha ile ambayo ni ya uongozi na ukarimu na wakusamehea na wa huruma ambayo siwezi kuishi bila—ambayo sitaki kusishi bila. Nataka kumuona Akiwa na nguvu. Nataka kumuabudu. Nataka kumuona na upendo. Nataka kumuona mwenye hekima kupita kiwango cha maneno. NA, NATAKA KUWA NAYE! Nataka kusikia kila neno analotaka kulisema. Sitaki kabisa kuwa hatua moja kutoka Kwake kwa maisha yangu yote. Siwezi kumgeuzia mgongo kwasababu ya uchoyo, maringo au uvivu au za hisia za kuumiza. Siwezi kumugeuzia mgongo. Majaribu yapo lakini kupoteza ni kuu sana.
Yesu anazo hizo sifa zote.Ako kwa njia1,000 tofauti na hekima kupita maneno. Huyu ni Mwongozi.Huyu ni Yesu. Hii sio hadithi. Hii sio hadithi huko nje juu ya miungu ambao waliumba dunia na kuketi juu ya kiti kikubwa cheupe cha enzi. Hii ni juu ya Utu wa Yesu na Baba Yake ambaye anatuongoza sisi wote. Tukiangalia,tukipata wasia wa kukutana naye, hakuna njia ya Kumzuia kabisa. Shida imekuwa ni ukosefu wa kujitolea na kutuwacha sisi wenyewe ndani ya uwozo na Mikono Yake ya ukweli.Ukweli wake ni zaidi ya uaminifu. Lakini kila wakati hatuendi karibu kuona, kwa sababu tunajiweka sisi wenyewe kuwa na kazi nyingi, wachoyo, kutojali sana—na hatutaki kuchukua wakati kuangaziwa au kuvutiwa naye.
Baba anajua kuwa tukichukuwa wakati kuwa naye ndani ya Mwanawe,Basi ataonyesha tabia yake kwetu kwa njia hii ambayo haitazuilika. Sifa za tabia Yake zinasitasita.Kuna kitu juu a kuwa Naye kitakacho kututua dhidi ya vitu vingine ambavyo vitakuwa mzigo na kukuvuta chini.Punde,unashangazwa na kitu ambacho kiko nje ya eneo la kuenea kwa ustadi wako. Naye ni YESU! Na, anatukaribisha kuja kutembea naye. Atakuangazia na sifa zake za utukufu,huruma na kusamehewa daima dawamu.
Utaona Akitabasamu na mwangaza katika macho Yake.Utaona vile upepo unavuma kupitia kwa nywele yake.Utaona, kusikia, na kushuhudia vitu ambavyo vitakupeleka hadi kwa eneo lingine, na wakati hautakuwa hapo tena(Ufunuo 1:12-18).Utaona uongozi Wake na nguvu Zake. Utaona vile Atakavyoamua dhidi ya dhambi. Utaona vile Ana mwelekeo na maono angavu ya vile maisha yanavyo stahiki kuwa. Na utasikia undani wa kicheko Chake na uhisi ujoto wa motisha na kukumbatiwa.
Njoo umfuate. Atakuonyesha uongozi. Atakuonyesha nguvu. Atakuonyesha tabia zisizo tingizika na hulka jinsi maisha yatakavyokung’arisha na kukufanya wewe kuja naye kwa sababu hautakuwa hatarini .Na uko mahala pema Alipo.Atakuonyesha ukarimu wake na unyenyekevu ambayo itakuelekeza katika roho na maisha. Ukija Kwake na utubu dhambi zako atakuosha na kukutakasa na kuweka roho Yake ndani yako.Sasa, atatoa almasi na yakuti na madini yaliyoko. Atatoa vitu hivyo,Atakufanya uwe malkia, Atakufanya uwe mfalme.
Anataka kujenga jeshi la wafuasi lakini sio la wale wasio hitimu ekevu kutumiwa kisheria—“Nifuateni au mtaenda jehanamu”. Hiyo ni kweli lakini halihusiki na yale Yesu alikuja kuonyesha wafuasi wake kumi na wawili. Je, unafikiri walimfuata Yesu kule kote mashambani alikoenda kwa sababu alikuwa anaonyesha kidole kwao na kuwaambia wamfuate au wataenda jehanamu? Je, unakumbuka maandishi kama hayo? Je ni hivyo ndivyo Alivyofanya alipoenda na kumwomba Baba usiku wote? Je, alisema Baba nionyeshe nitakalo sema na akasimama na akasema “nyinyi wafuasi wangu kumi na wawili njooni nami au mtaenda jehanamu?” Hapana.Walitaka kuwa Naye kwa sababu waliona kitu kumhusu ambacho kuliwashangaza, waliona hekima Zake na uvumilivu. Waliona uongozi dhabiti na tabia zisizobadilika.Waliona mtu ambaye atachukuwa upigo wa maisha na kusimama wima pamoja na kicheko kidogo kwa uso wake, na ujasiri kwa macho Yake. Na walitaka kuwa kama yeye—. Walitaka kuwa naye! Hawakuwa wanaenda mahala popote kwa sababu hapakuwa na mahali popote walitaka kwenda ila kuwa kando Yake (Mathayo 4:19-22,Yohana 5:68 Matendo 5:20, Matendo 3:19-20)
Hakutaka kuwaugofya na Hatuogopeshi sisi pia. Anatukaribisha kumwona Yeye kama vile alivyo na kuona maajabu ya matendo na maajabu ya ubihafsi yale aliyonayo….ili ndiyo tuwe Naye, kwa maisha haya na yajayo.Ningependa niwe kama Yeye nikiwa mkubwa.
Kabla mda mrefu Yesu atakuja kumchukuwa bi harusi ambaye yuko tayari. Naye, kwa kutaka kwake Baba kwetu si kuhudhuria bi harusi bali ni kuwa bi harusi….si kuhudhuria nyumba bali ni kuwa nyumba.Ukirejelea Agano La Kale, utaona haja Yake imekuwa na nyumba; bali si ya waliokolewa kwa kutaka kwake ila kupenda kwake kwa mahala ambapo Angeishi hapa duniani Aliyoumba. Yesu anatuambia katika kitabu cha Luka 17 ya kuwa ulimwengu Wake hauko hapa au pale, lakini uko ndani ya watu waliopanua mahala pa nyoyo zao, kuondoa mambo ya ulimwengu, hisia za kimwili hamu na ndoto ni lazima tuwe wale walitegeneza nafasi ya Yesu katika nyoyo zetu kama vile Yesu alivyotufunza katika kitabu cha Yohana 8. Na hiyo ni maumbile ya Ekklesia mwili wake unavyoishi na kanisa.
Yesu hakuja kusamehe dhambi kwa uzuri kama huo au kutufanya tufikirie juu ya mafunzo Yake. Yesu alikuja ili tujuwe maisha yaliyvo sawa na Baba ambayo alishudia—sio tu kuishi hapa, kufa, na tena kupaa mbinguni. Kama vile Bibilia inavyosema, alikuja hapa ndivyo tuishi “kwa nguvu ya maisha Yake yasiyo haribika” kushudia usawa wa ushirika na maisha na upendo pamoja na baba na nduguze vile Yesu alivyofanya.
“Kuokoka” ni MBALI sana na mwisho wa hadithi.Kulingana na kuzaliwa kwa Yesu, kuzaliwa kwetu Ni Kianzo tu cha hadithi ambayo Baba anataka kusema ndani yetu (Wakolosai 1:26-29, Wagalatia 4:19, Yohana 7:37).Nia au mapenzi Yake ni kwamba Yesu ametengenezwa ndani yetu na kwamba sisi (watu wote, Bi Harusi, Nyumba Yake) zitakuwa dhibitisho ya Utukufu wa Yesu wa Nazerethi hapa duniani wa kisasa. Katika ziku hizo. Nia ya Mungu siyo kwamba Yesu aonekane ndani yao, lakini ati kwa PAMOJA, muungano na tutaweza kuwa waakilishi wa Yesu.
Na, kufanyika kwa hayo yote “kutafuta utajiri” uko na kila kitu kuhusu vile tunaishi maisha yetu ya kilasiku pamoja. Mengi ya dini na Ukristo zimefanywa kwa miaka mingi ni kutufunza maandiko kumhusu Yesu na Kanisa.Ni wakati wa kuendelea kujifunza mafunzo ya Kanisa na uumbile wa kanisa.(Waefeso 3:10, Mathayo16:18)
Tunaweza TU kuwa kanisa Lake na kuishi maisha Yake tunapopendana na kubadilisha maisha yetu na wengine kila siku. Tunasaidiana kumjua Yesu vizuri kwa kusaidiana, kuepukana na dhambi, kupendana na wengine, na kujali maslahi ya wengine. Vile tunavyo jijali. Haya ni mafundisho ya Yesu. Hivi ndivyo alivyoishi maisha yake kwa ajili ya sisi na ametuita tuishi hivyo kwa ajili ya wengine. Hivi ndivyo Bi harusi anavyo “tayarishwa” kwa kurudi kwa bwana Harusi Yesu. Kila mara tunakuwa warembo tunavyo jifunza jinsi ya kupendana kwa ukweli. Tunapoweka kando ile ubinfsi na maringo yetu inayotugawanyisha na wengine, na tunapo fungua mioyo yetu ionekane na wengine, Roho mwema, wema wa Mungu na upendo wa Mungu unamwagika juu yetu…. na tunafanywa Bi harusi aliye tayari kwa kurejea kwa Bwana Yarusi Yesu Kristo.
Hili ni Kanisa—kuishi hivi kila siku, kutohudhuria nyumba ya Mungu, lakini kuwa mahali Mungu anaishi. Kwa hivyo nyumbani kwetu, mahali petu pa kazi, na Kanisa letu lote zipo pamoja. Hakuna tena vizuizi ndani ya roho yangu kwako na hakuna vizuizi katika ya nyumba yangu na yako. Naweka kando ubinafsi, maringo,uvivu na kutoamini na ninawapenda wengine jinsi Yesu alivyo nipenda mimi. kila mtu anapofanya hivyo, kutoka kwa mdogo hadi mkubwa yesu anatumwagia mafuta ya uponyaji na tunakuwa kanisa. Bi harusi mrembo. Yesu hakuja kutufanya sisi kuwa werevu. Alikuja kutupa maisha kikamilifu—Kuishi maisha yake kilasiku kati yetu, sio kutamka maneno yaliyo ombwa, kuimba nyimbo na kuomba maombi yalivyo ombwa, kuimba nyimbo na kuomba maombi yalivyochafuliwa k.m. kioo kilichochafuliwa.MAISHA!