UONGOZI WA YESU

KATIKA WATU WAKE WOTE

Hakustahili kuwa na wakubwa rasmi ambao wanasimamia maamuzi, pesa, na watu—isipokuwa Yesu na kupitia Watu Wake pamoja na Roho Yake. Wale Wake wote waliobadilishwa na Yeye anaishi ndani yao, kwa kuishi Maisha ya kila siku iliyotakaswa kwa pamoja na wanaonekana ni Wake (Waeb. 3:12-14)—WOTE ni Makuhani!

7/5/2006

Yesu nyumba kanisa

Wakristo wa uongo kwa miaka mingi wamewasukuma watu chini. Imewachukua watu wachache na kuwasukuma juu hivyo basi kuwafanya “viongozi” wengine matajiri na wenye kujulikana sana na wenye nguvu, i hali wana wasukuma watu wengi chini. Marekani, India, uholanzi, Romania, Brazili, na ulimwenguni kote, kuna Wakristo “mashujaa” na Wakristo wa “chini.” Hii ni vibaya sana. Yesu aliwaambia watume kumi na wawili katika Mathayo 23 “Usimwite mtu ye yote mwalimu, usimwite mtu yeyote baba, usimwite mtu yeyote kiongozi, usimwite mtu yeyote bwana, usimwite mtu yeyoye ‘rabi’, usimwite mtu yeyote ‘mchungaji’, usimwite mtu yeyote ‘mheshimiwa’—kwa kuwa nyinyi wote ni ndugu mlio na Baba Mmoja!” Hakuna “mashujaa” katika Ukristo wa Kweli isipokuwa Yesu. Hakustahili kuwa na wakubwa rasmi ambao wanasimamia maamuzi, pesa, na watu—isipokuwa Yesu na kupitia Watu Wake pamoja na Roho Yake.

Biblia inasema katika Waefeso 4 kwamba wakati Yesu alienda Mbinguni na akatuma Roho Wake, Alichukua sehemu zake Mwenyewe na kuzigawanya kwa Mwili wa Kristo, Kanisa. Yesu alichukua vipawa vyote alivyokuwa navyo ( na Yesu alikuwa na vipawa vingi vya kiroho, sivyo?) na akawapa watu Wake wote. Hakuchukua vipawa vyote alivyokuwa navyo na akampa “mchungaji” au “mtu mmoja wa Mungu.” Maandiko yanasema Alichukua Vipawa Vyake vyote na akavipa mwili Wake wote. Biblia inasema Roho huwekwa na kupeanwa kama Kipawa, kama vile Roho apendavyo, kwa Kanisa lote. Ikiwa wewe ni Mkristo wa kweli, ikiwa kwa kweli umeacha maisha yako kwa ajili ya Yesu, basi Roho Mtakatifu hukupa wewe kipawa maalum sana.

Na, kipawa chako ni sehemu ya Yesu. Kuna vipawa vya aina nyingi sana vilivyoorodheshwa kwenye Biblia. Kwa mfano, Roho Mtakatifu hupeana neema kama kipawa. Kipawa cha neema ni sehemu ya Yesu ambayo aliwapatia watu wengine. Ni kipawa kisicho cha kawaida. Sisi wote tunapaswa kuwa na neema, sivyo? Lakini kuna neema isiyo ya kawaida ambayo ni kipawa cha Roho Mtakatifu. Na kwa kuwa mamlaka yote ni ya Yesu na kila kipawa ambacho kila mmoja wetu anacho ni sehemu ya Yesu, basi tunanyenyekea kwa vipawa ambavyo viko katika kila mmoja wetu kwa sababu ni Yesu alivitoa.

Kwa njia hii, uongozi uko katika watu wote wa Mungu. Biblia hutuita sisi Ufalme wa makuhani. Biblia haisemi Ufalme ulio na makuhani, bali Ufalme wa makuhani. Hakuna kikundi maalum kama vile makuhani Walawi wa Agano la Kale. Katika Agano Jipya, watu wote wa Mungu wanapaswa kuwa kuhani wa yule mwingine. Kusudi la Mungu si mtu mmoja maalum mtakatifu ambaye anaweza kuhubiri. Biblia inasema Yesu alipaa juu na akapeana Vipawa Vyake kwa watu Wake wote. Alifanya Ufalme wa makuhani. Aliweka sehemu Zake katika kila mtu Wake ambaye kwa kweli amebadilishwa, kijana au mzee. Hiyo ndio maana tuna hitaji vipawa vya yule mwingine. Tuna hitaji vipawa vyote vya Yesu! Kuna mamia ya vipawa kwa sababu VYOTE vya Yesu vilimwagwa kwa Familia Yake. Hii ndio maana Yesu alisema sisi wote ni ndugu kati ya ndugu. Hatuhitaji mtu mmoja na kipawa kimoja kikisimama mbele yetu tena. Tusiruhusu hiyo tena. Wale Wake wote waliobadilishwa na Yeye anaishi ndani yao, kwa kuishi Maisha ya kila siku iliyotakaswa kwa pamoja na wanaonekana ni Wake (Waeb. 3:12-14)—WOTE ni Makuhani!

Hakuna mamlaka fulani maalum ambayo yako kwa “mtu mmoja wa Mungu” na wale wengine wote wanakaa na kumtazama. Kwa sababu ya vile wanadamu wamejenga kanisa kwa miaka 180o na zaidi iliyopita, tumefanya kana kwamba kuna kipawa kimoja—kipawa cha “uchungaji.” (Au pengine kila mtu yeyote ameruhusiwa kuwa na “kipawa cha kutoa pesa”!) Lakini uchungaji ni kipawa kimoja tu! Tukijenga vibawa, sisi wote tunapoteza. Ikiwa mtu mmoja amesukumwa mbele ili awe “mchungaji” na kila mtu mwingine anakaa chini na kusikiliza kila wakati, basi hakuna yeyote anaushiriki na kipawa chako. Wanapata vipawa vya “uchungaji” tu. Hiyo ni kidogo sana na iharibikayo! Ikiwa tunataka kuona ukubwa wa Mungu, na ikiwa tunataka kuona maisha yetu yote yakibadilika na maisha ya watoto wetu yakibadilika, tunahiji VYOTE vya Yesu. Vipawa ambavyo kila dada na ndugu anavyo ni sehemu ya Yesu. Hata watoto wana vipawa ambavyo ni sehemu ya Yesu. Tunahitaji vipawa hivyo vyote katika maisha yetu. Sisi wote ni ndugu. Moyo wa Mungu ni kuwa nipewe kipawa ambacho unacho na nikupe kipawa ambacho ninacho. Tusitosheke tu na sehemu ya Yesu. Amina?

Je! unaona ni kwa nini tulisema ni lazima uwe na ujasiri? Mambo lazima yabadilike! Hauwezi kuendelea kuyafanya yale ulikuwa ukiyafanya. Itakubidi uamue kutumia vipawa vyako zaidi na kuwakaribisha wengine wafanye hivyo pia. Itakubidi uamue kuwa mtiifu na uwe na ujasiri. Ukiendelea kukalia kiti chako au kukaa sakafuni kila wakati na usitumie vipawa vyako zaidi ya vile ulivyokuwa ukivitumia, vipawa vyako vitaendelea kupotea. “Yule ambaye amepewa imani au kipawa lazima awe mwaminifu.” Je! unakumbuka kilichomfanyikia mtu yule ambaye alizika kipawa chake? Yesu alisema, “Wewe mtumishi muovu, mvivu.” Hivyo ndivyo Yesu hutuambia wakati tusipofanya kile tunachopaswa kufanya. Nikikosa kutumia kipawa changu au ukikosa kutumia kipawa chako, tunakuwa “waovu na wavivu.”

Je! ikiwa wewe ni mkimbiaji wa Olimpiki na umelala kitandani na mtu akachukua kamba na akakufunga? Ijapokuwa unaweza kuwa bingwa wa riadha, ukifungwa kitandani misuli yako itapungua, na mwishowe utakufa. Uwezo wako wote utapotea kwa sababu umefungwa kwa kitanda kwa miezi au miaka. je! unaona vile tamaduni za wanadamu zimeiba na kufunga Neno la Mungu? Vile tulivyojenga kwa zaidi ya miaka 1800 katika Nyumba ya Mungu imefunga watu wengi wa Mungu kwa kitanda! Hawajaweza kuamka na kukimbia na kutimiza umilele wao kwa sababu wanadamu wamejenga vibaya, hawajafuata Neno la Mungu. Tukijenga au kuunda kanisa kwa njia ambayo inamwinua mtu mmoja au “mfanyakazi” na kumaliza vipawa vya wengine, sisi ni waalifu katika Mahakama za Mbinguni kwa sababu ya uharibifu na hasara ambayo wengi watapitia kwa sababu ya “chachu kwenye mkate” na Vipawa visivyotumiwa!

Sio kwa sababu watu ni “wabaya” ndiposa tumekuwa tukijenga vibaya. Mara kwa mara ni kwa sababu hatukujua njia ya kujenga Nyumba ya Mungu na Mbuni ya Mungu. Kwa miaka 1800, ulimwengu wa Wakristo umechanganya masuala ya Mkristo ni nani… kiongozi ni nani… vile maisha ya kila siku inapaswa kuwa… na vile mikutano inapaswa kuwa. Baba yetu anataka kurudisha vitu hivi katika maisha yako sasa. Kama vile Neno la Mungu lilikuwa limepuuzwa katika siku za Mfalme Yosia, na Kweli ilipatikana imezikwa katika kifusi cha falme na tamaduni za wanadamu, kwa hivyo leo Ukweli wa Mungu, ulipuuzwa kitambo (lakini kila mara katika Biblia) unaweza kumweka mwanadamu huru. Mungu atabadilisha maisha yako kwa kimiujiza na kubadilisha kila mmoja karibu na wewe kama matokeo yake. Hii ni kweli yenye nguvu na ya dhamani sana. Aidha kuna chache au nyingi katika mji wako au boma, “Mungu hazuiliwi kuokoa wengi au wachache” kama vile Jonathani, rafiki wa karibu wa Daudi alivyosema. “Yule aliyepewa imani lazima awe mwaminifu.” Lazima tuwe na ujasiri wa kufanya jambo kuhusu Ukweli tuliopuuza au tuliokosa kutii zamani. Na Yeye Mwenyewe atakuwa Mchungaji wako, Ngome yako, na Mlinzi wako unapomwishia kwa ujasiri.

jesuslifetogether.com
Kiswahili Languages icon
 Share icon