UONGOZI WA YESU
SAMWELI DHIDI YA SAULI
“Kuwa kiongozi” hutokana na uhusiano na Mungu na watu wa Mungu. Sio kutokana na ofisi au jina.
7/5/2006
Katika nchi zote duniani kote, sisi wote tumefanya makosa makubwa sana kuhusu uongozi kanisani. Katika sehemu nyingi mtu ambaye amesomea Biblia katika chuo cha Biblia au shule za biblia, au mwanabiashara mzuri au mnenaji, anakuwa kiongozi au “mchungaji.” Tumeona nchini India na nchi zingine, wakati mwingi, kwamba mtu aliye na baisikeli ambaye anaweza pia kusoma anachaguliwa kuwa kiongozi. Hii sio njia ya Mungu! Uongozi wa Mungu msingi wake si yule anayeweza kusoma, au yule anayejua zaidi, au yule anayeweza kuzungumza vizuri kabisa, au yule ambaye ana ujuzi bora kabisa wa biashara, au yule ana mali au elimu au anayependeza au kuvutia au baisikeli.
Wacha nikufafanulie aina ya viongozi wawili tofauti kabisa. Mmoja ni kiongozi kutoka moyoni, kutoka kwa uhusiano wa sasa na Mungu. Mwingine ni kiongozi wa cheo ambaye anaweza kuwa na jina na anaweza kuwa mkubwa “mtu mkuu,” mkubwa rasmi. Yesu alisema kwamba haipaswi kuwa kiongozi kwa cheo. Viongozi wa Kanisa ni wale ambao wanatembea kwa karibu sana na Mungu KILA SIKU. Ikiwa ndugu au dada hatembei kwa karibu sana na Mungu kila siku, hawezi kuzingatiwa kuwa kiongozi. Ikiwa pengine mtu wiki iliyopita hakuwa karibu na Mungu lakini ametubu dhambi katika maisha yake na sasa anaweza kumsikiza Mungu vizuri, yeye ni kiongozi zaidi wiki hii zaidi ya wiki iliyopita. “Kuwa kiongozi” hutokana na uhusiano na Mungu na watu wa Mungu. Sio kutokana na ofisi au jina. Tuna viongozi wengi katika mji tunapoishi, lakini hatuna “maafisa.” Kiongozi wiki hii anaweza kuwa si kiongozi wiki inayofuatia. Yesu alisema mamlaka yote mbinguni na duniani ni YAKE. Hii bado ni kweli. Kwa hivyo, ijapokuwa tunaweza kumsikia Yesu, ambaye ana mamlaka yote, hayo ndiyo mamlaka ambayo mwanadamu anayo—sawa tu na vile anavyoweza kumsikia Yesu. Hiyo imetosha. Alisema, “Mamlaka yote Mbinguni na duniani” ni ya Yesu. Mtu ambaye hajui au kumtii Yesu anaweza kuwa “sanamu” tu. Mtu kama huyo anaweza kutiiwa kulingana na vile dhamira inavyoruhusu, ikiwa ana “cheo,” lakini yeye ni “kiongozi” tu kulingana na vile anavyojua, anavyopenda, na kutii Kichwa, Yesu.
Kwa kweli kuna mfano katika Biblia ya aina ya viongozi hawa wawili tofauti kabisa. Samweli na Sauli walikuwa viongozi wa watu wa Mungu, Israeli. Samweli alikuwa mtu wa Mungu ambaye alikuwa na ushawishi katika taifa hilo kwa sababu alimjua Mungu. Samweli alikuwa na tabia zote za Mfalme wa Israeli—lakini Samweli hakuwa mfalme! Walakini, Sauli aliitwa mfalme. Israeli ilitaka kuwa na mfalme—walitaka kuwa na mtu mmoja awe mkubwa. Walitaka mtu wa kubadilishana na Samweli, na walitaka”mfalme” kama vile mataifa yaliyowazunguka. Kwa njia hiyo moja uongozi unaweza kuonekana unafanana, lakini Samweli hakuwa na “cheo” cha mamlaka. Samweli alifanya kazi kutokana na uhusiano wake na Mungu, na Sauli akafanya kazi kutokana na cheo/ofisi yake. Samweli hakuwa na ofisi, katibu, au mshahara. Hakuwa katika “cheo cha mfanyakazi” kama mfalme. Samweli alikuwa mtu wa Mungu ambaye aliheshimiwa kama mfalme, lakini hakuwa na ofisi wala cheo. Hakuwa mfalme. Hakuwa “mchungaji.” Alimpenda Mungu kwa moyo wake wote. Na kwa sababu angeweza kumsikia Mungu, alikuwa na ushawishi. Hakuwa na cheo…alikuwa na ushawishi. Ikiwa mtu kwa kweli anamjua Mungu, atawasaidia watu wa Mungu. Ikiwa ameitwa na Mungu, atakuwa akiwasaidia watu. Nitaisema tena: Mtu wa kweli wa Mungu hana cheo… ana ushawishi. Ayubu, 29, ni ufafanuzi wa mtu aliyeheshimiwa na Mungu na wanadamu, na aliogopwa na kuchukiwa na shetani. Mtu kama huyo haitaji afisi au jina au mshahara. Ikiwa wewe ni kama Yesu, hauhitaji “nguvu” zozote.
Kwa mfano, ikiwa mimi ni seremala, ninatengeneza vitu kwa mbao. Ninatengeneza kiti, meza, au mlango kutoka kwa mbao ikiwa mimi ni seremala. Ikiwa mimi ni mwashi, basi ninatengeneza vitu kwa matofali. Kitu nilichokiunda kutoka kwa matofali ndiyo dhibitisho la kuwa mimi ni mwashi. Kitu nilichokiunda kutoka kwa mbao ndicho dhibitisho la kuwa mimi ni seremala. Hivyo pia, katika Biblia neno “mchungaji” (kwa kweli, tafsiri mbaya) hurejelea kipawa cha mchungaji, kinachotumika kila siku kati ya watu wa Mungu pamoja na vipawa vingine—sio ukubwa au “kichwa kinachozungumza” wakati wa mkutano. Je! dhibitisho liko wapi la kuwa mimi ni mchungaji? Dhibitisho ni kuwa nina wapenda watu wa Mungu! Nina wasaidia mchana na usiku. Si hitaji ofisi kufanya hivyo. Si hitaji jina. Si hitajiki kuwa mkubwa. Nina wapenda watu kwa kipawa ninacho, na nina wasaidia. Dhibitisho la kuwa mimi ni seremala ni kiti nilicho kiunda. Dhibitisho la kuwa mimi ni mchungaji ni kuwa nina walisha watu wa Mungu kila siku, na wako karibu na Yesu kwa sababu yangu. Nikiona mmoja wa watu wa Mungu ana njaa, inavunja moyo wangu. Nikiona kwamba mmoja wa watu wa Mungu yuko taabani au hatarini, moyo wa mchungaji ndani yangu huwakimbilia ili kuwalinda. Hilo ndilo dhibitisho la kuwa mimi ni mpakwa mafuta wa Mungu ili niwe mchungaji. Sihitaji tepe ya jina. Sihitaji cheti kwenye ukuta na diploma kutoka kwa chuo cha Biblia. Nina hitaji moyo wa kupenda na kufanya kazi ya Mungu, na kwa hivyo nita zaa matunda ya kitofauti katika eneo lolote ambalo amenipatia kipawa.
Kwa hivyo, wewe ni seremala? Hivyo basi tengeza viti. Una kipawa cha uchungaji? Basi wapende watu—kwa kuwalisha, kuwalinda, na kuwasaidia. Hii ni kweli kwa kipawa chochote! Dhibitisho la kipawa chochote ni katika tunda linalo zaa.
Kwa hakika, kinyume cha haya yote pia ni kweli. Ni ukweli wa ajabu kwamba wapagani katika fani ya sayansi na madawa kwa kweli hudai kwamba wale walio na maoni na ufafanuzi na wanaojidai “wataalam” wana kitu cha kuonyeshana, tunda fulani katika maisha yao, la kuonyeshana kwamba wana haki ya kuwa papa au kufunza au kuwashutumu wengine. Katika ulimwengu wa kidini, la kushangaza, kuna uadilifu mdogo zaidi ya vile wapagani wanavyoonyesha. Walakini, katika dini, watu mara kwa mara ni vipofu zaidi na wanapendelewa. Ukosoaji, utaalam, hukumu, na hata pia uhujumu wa uhusiano na uzushi humiminika virahisi kutoka kwa wale walio na tunda bovu katika maisha yao, familia zao, na mikusanyiko yao. Ya kushangaza zaidi, lakini kweli, ukitazama dini ya mtu kwa makini na kwa uaminifu. Mtu anayefanya vitu kama hivyo kama vile kudanganya au uzushi au anayefanya kama mtaalam wa uhandisi au madawa, au biashara kwa kweli anaweza kufungwa. Lakini, katika dini wanaweza kwa urahisi kukusanya umati kati ya waogopao au wasiojua au wale ambao wanaweza kushurutishwa, kusalitiwa, au kusifiwa ili wakubali mashine isiyozaa matunda na “wataalam.” Ya kushangaza, lakini ni kweli. Hufanyika kila wakati, kwa sababu hivyo ndivyo ufalme wenye makosa uhifadhi watu wake. Uoga na sifa, masengenyo, chongezi, uzushi, au usaliti wa kihisia. Haishangazi kwamba Yesu hakufanya vyema katika dini za siku Zake zilizokuwa duniani. Lakini, tunaweza kujifunza kutoka Kwake na kukumbatia Andiko, na kutafuta Tunda, wala si sikia-sema na ajenda na mifupa iliyofichwa, bajeti, na kiburi cha kulinda.
Kwa kweli, sasa unapata wazo hilo. :)